John 19:17-22

17 aIsa, akiwa ameubeba msalaba wake, akatoka kuelekea mahali palipoitwa Fuvu la Kichwa (kwa Kiebrania ni Golgotha). 18 bHapo ndipo walipomsulubisha. Pamoja naye walisulubisha watu wengine wawili, mmoja kila upande wake, naye Isa katikati.

19 cPilato akaamuru tangazo liandikwe na liwekwe juu kwenye msalaba wa Isa, likasema: “Isa Al-Nasiri, Mfalme wa Wayahudi.” 20 dKwa kuwa mahali hapo Isa aliposulubiwa palikuwa karibu na mjini, Wayahudi wengi walisoma maandishi haya yaliyokuwa yameandikwa kwa lugha za Kiebrania, Kiyunani na Kilatini. 21 eViongozi wa makuhani wa Wayahudi wakapinga, wakamwambia Pilato, “Usiandike, ‘Mfalme wa Wayahudi,’ bali andika kwamba, mtu huyu alisema, ‘Mimi ni mfalme wa Wayahudi.’ ”

22Pilato akawajibu, “Nilichokwisha kuandika, nimeandika!”

Mavazi Ya Isa Yagawanywa

Copyright information for SwhKC